Brice Juliusjoram
Mimi ni mfanyabiashara kwahiyo tukutane katika kujadiliana kwa kina katika kupanua biashara zetu. Mungu awabariki sana.
Brice Juliusjoram
Jumatatu, 6 Februari 2017
Jumanne, 3 Januari 2017
JE WAJUA MAANA YA NENO X-MAS NA CHRISTMAS?
Je, wajua tofauti ya kati ya neno {CHRISTMAS} na
neno {X-MASS }?
Kama hujui soma hapa:
👇👇👇👇👇👇👇👇
CHRISTMAS ni MUUNGANO wa maneno mawili yaani CHRIST & MAS.
Hapo zamani, siku ya Tarehe 25 December, ilikua siku ya Kusherehekea MITAMBIKO YA KIPAGANI kabla MWANA WA MUNGU, YESU KRISTO hajazaliwa.
Baadae mwaka 533 AD, Mtakatifu Constantine, aliyekua Mkuu wa Kanisa la WARUMI, ambalo siku hizi linajulokana kama Kanisa la Katoliki (Kanisa la kwanza), aliibadili siku hiyo isiwe tena ya MITAMBIKO YA KIPAGANI badala yake siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa MKOMBOZI MWANA WA MUNGU YESU KRISTO na kuiita siku ya kusanyiko la KRISTO yaani CHRISTMAS.
1. CHRIST ni neno la kiingereza ambalo tafsiri yake ni KRISTO yaani MASIA au MPAKWA MAFUTA au ALIYETENGWA KWA KAZI MAALUMU.
2. MAS ni neno la KIYUNANI ambalo maana yake ni KUSANYIKO.
Kwa hiyo maana ya neno CHRISTMAS ni KUSANYIKO la KRISTO.
Kwa WAKRISTO wanaoamini siku hiyo, wawe makini sana na neno X-MASS!.
Inaaminika kuwa, baada ya siku hiyo ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO, kupata umaarufu, neno X-MASS, lilikuja baadae sana na lililetwa na wapinga KRISTO ambao waliamua kufuta neno CHRIST kwa kuweka alama ya "X" yaani hakuna KRISTO.
Hiyo ilibadili maana kwa kusomeka X-MASS.
X-HAKUNA na MASS-KUSANYIKO, hivyo X-MASS, maana yake ni HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO! yaani HAKUNA CHRISTMAS!
Sasa, Kama wewe ni Mkiristo hutakiwi kutumia neno X-MAS, badala yake tumia neno CHRISTMAS
MUNGU awabariki muwe na CHRISTMAS Njema sio "X-MASS!"
...... By.........
Brice J.Joram
Jumamosi, 31 Desemba 2016
Ijumaa, 30 Desemba 2016
Naumiliki mwaka 2017
Bwana Yesu kristo asifiwe Sana wapendwa katika Bwana.
Ninafuraha kubwa kumshukuru Mungu kwa yote natumaini Mungu mwema ametufikisha leo Trh. 31 tukiwa na pumzi. Wapo wengi tulianza nao lakini wameishia Katikati hawakuweza kumaliza mwaka.
Tukumbuke haikuwa rahisi ila ni rehema na Neema za Mungu kwetu ametushindia kwa ushindi wa ajabu hatuna cha kumlipa zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.
Haijalishi mwaka 2016 umepitia mangapi magumu na mazito lakini umevuka Salama jua tambua kuwa si nguvu zako ila ni rehema zake Mungu.
Hivyo basi tuungane kwa pamoja siku ya leo kutafakari matendo makuu ya Mungu aliyo tenda mwaka 2016 na pia kumkabidhi mwaka 2017 anze pamoja nasi.
Immanuel Mungu pamoja nasi awa nawe Kwanzia sasa na Hata milele Amen.
Mungu awabariki sana na awape umaliziaji mwema wa masaa Haya machache yaliyo baki na tupokee mwaka Salama.
Katika jina la Yesu kristo Amen.
HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA.
......... By. .........
Brice J.Joram
Jumapili, 25 Desemba 2016
Yesu Kanikombia
Nawatakia kheri ya mwaka mpya Na Mungu awabariki sana pamoja na kuwawezesha katika kufanikinisha malengo yenu 2017 na uwe mwaka Wa mafanikio tele. Pia Mungu azidi kutufundisha kwa kina zaidi.
................by...........
**BRICE J.JORAM**
Ijumaa, 23 Desemba 2016
Kheri ya Christmas & Happy New Year
Makao makuu ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Dar mwinekano Wa maandalizi Christmas na Happy New Year
...............by...........
****BRICE J.JORAM****
Alhamisi, 22 Desemba 2016
Kheri ya Christmas na Happy New Year.
Mungu awape mwongozo mwema Wa maisha yenu katika mwaka 2017 na awafanikishe katika kazi zenu.
Pia Mungu awafungulie milango ya fedha kwa wingi katika mwaka ujao 2017 ,awape kila muliombalo kwake .
..................by..................
BRICE J.JORAM